Monday, March 31, 2014

M-pesa yanogesha maadhimisho ya ustawi wa wajamii

Naibu Waziri wa Afya Dk. Steven Kebwe akicheza midundo ya kikundi cha sanaa cha watu wenye ulemavu cha Chuo Cha Ufundi Yombo wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Ustawi wa Jamii Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Chuo Cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama, Jijini Dar es salaam. Maadhimisho hayo yanaratibiwa na  Chama Cha Wanataaluma ya Ustawi wa Jamii (Taswo) 

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akiwatuza wasaanii wa kikundi cha watu wenye ulemavu wa Chuo Cha Elimu ya Ufundi cha Yombo wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Ustawi Duniani yanayofanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama Dar es salaam.

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akitoa salaam za kampuni yake wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Ustawi duniani inayofanyofanyika katika viwanja vya chuo cha Ustawi, Kijitonyama jijini Dra es salaam. Maadhimisho hayo yanaratibiwa na Chama Cha Wanataaluma ya Ustawi wa Jamii (Taswo)
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Steven Kebwe akiteta jambo na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim( kushoto) wakati akielekea jukwaa kuu tayari kuongoza uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Ustawi wa Jamii. Maadhimisho hayo yanafanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Taswo Dk.Zena Mabeyo

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Steven Kebwe (kulia) akipewa maelezo na Mwezeshaji wa kikundi cha wajasiriamali kutoka Karatu Jane Mwelye,wakati alipotembelea banda lao katika maadhimsho ya wiki ya Ustawi katika viwanja vya chuo cha ustawi wa jamii jijini Dar es Salaam.Katikati anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalimu

No comments:

Post a Comment